Skip to content

twarc1

=====

twarc ni chombo ya command-line na Python Library ya kuhifadhi Twitter JSON data. Kila Tweet ita akilishwa kama kitu ya JSON ita onyeshwa hivi kutoka kwa Twitter API. Tweets zita wekwa kama line-oriented JSON. twarc ita kusaidia ku chunga rate limits ya API ya Twitter. twarc pia ita sanya tweets, watumiaji wa Twitter, uwenendo za Twitter na ita hydrate tweet ids.

twarc imeundwa kama sehemu ya Documenting the Now ambayo ilifadhiliwa na Mellon Foundation.

Weka

Kabla kutumia twarc utahitaji kujiandikisha kwa apps.twitter.com. Mara baada ya kuunda programu yako andika consumer key and consumer secret yako alafu bonyeza kuzalisha access token na access token secret. Uta hitaji hizi vigezo nne ku tumia twarc

 1. weka Python (2 or 3)
 2. pip install twarc (ama kuboresha: pip install --upgrade twarc)

Haraka Haraka

Utahitaji kuambia twarc vifunguo ya API ya Twitter

twarc configure

alafu jaribu kuchungua na:

twarc search blacklivesmatter > search.jsonl

Ama wataka kusanya ma tweets kama zinatoka

twarc filter blacklivesmatter > stream.jsonl

Endelea kusoma ku pata maelezo kuhusu utumizi wa twarc

Matumizi

Sanidi

Mara tu una vifunguo vya Twitter unaweza kuambia twarc ukitumia command ya configure.

twarc configure

twarc ita andika sifa zako kwenye file itayo itwa .twarc kwa saraka ya home. Kama hutaki ama huwezi kuandika file hiyo unaweza kutumia command inayo tumia mazingira yako. (CONSUMER_KEY, CONSUMER_SECRET, ACCESS_TOKEN, ACCESS_TOKEN_SECRET) ama chagua command line (--consumer_key, --consumer_secret, --access_token, --access_token_secret).

Uchunguzi

Hutumia uchunguzi wa tweets kupakua tweets zilizoandikwa zinazo swala

twarc search blacklivesmatter > tweets.jsonl

Ni muhimu kukumbuka swali yako ita pakua tweets za mda wa siku 7 inayo tiwa na API ya Twitter. Kama swali yako inataka mda wa siku nane au zaidi waeza kutumia filter ama sample commands kama hizi.

Njia bora ya kujifunza na uchunguzi wa Twitter Search API ni ku jaribu Twitter's Advanced Search alafu kuitumia kwa twarc. Kwa mfano hapa tuna tafuta ma tweets zinazo #blacklivesmatter ama

blm hashtags zilizo tumwa kwa deray.

twarc search '#blacklivesmatter OR #blm to:deray' > tweets.jsonl

Twitter hujaribu kuweka lugha ya tweet na unaweza kupunguza kikoma yako kwa lugha ukitaka

twarc search '#blacklivesmatter' --lang fr > tweets.jsonl

Unaweza pia kutafuta tweets za mahali fulani kwa mfano tweets zinazo taja blacklivesmatter zilizo maili 1 kutoka katikati ya Ferguson, Missouri:

twarc search blacklivesmatter --geocode 38.7442,-90.3054,1mi > tweets.jsonl

Ikiwa swali yako haina maneno lakini umetumia --geocode utapata tweets zote za eneo hio.

twarc search --geocode 38.7442,-90.3054,1mi > tweets.jsonl

Chuja

Utumizi wa filter command husanya tweets zikiandikwa no hutumia statuses/filter API.

twarc filter blacklivesmatter,blm > tweets.jsonl

Tafadhali kumbuka kuwa syntax ya Twitter ni tofauti na Twitter ya uchunguzi. Tafadhali wasiliana na nyaraka jinsi ya kueleza chujia unayo tumia

Tumia command ya follow kama wataka kusanya tweets kutoka kwa mtumiaji kama zinatokea. Hi inajumuisha retweets. Kwa mfano hii itasanya tweets na retweets za CNN:

twarc filter --follow 759251 > tweets.jsonl

Waeza kusanya tweets kwa kutumia sanduku linalozingatia. Kumbuka: dash inayoongoza inahitaji kutoroka katika sanduku linalozingatia ama ita fasiriwa kama command line argument!

twarc filter --locations "\-74,40,-73,41" > tweets.jsonl

Ikiwa unachanganya chaguzi yako au OR'ed pamoja. Kwa mfano hii ita sanya tweets zinasotumia blacklivesmatter ama blm na pia tweets kutoka mtumiaji CNN:

twarc filter blacklivesmatter,blm --follow 759251 > tweets.jsonl

Sampuli

Tumia sample command kusikiliza kwa sampuli ya Twitter statuses/sample statuses hivi karibuni

twarc sample > tweets.jsonl

Punguza maji

twarc ina dehydrate command ita tengeneza orodha ya id kutoka faili ya tweets:

twarc dehydrate tweets.jsonl > tweet-ids.txt

Hydrate

twarc pia ina hydrate command ita soma faili inayo id na ita andika faili mpya ya tweet JSON kwa kutumiya Twitter status/lookup API.

twarc hydrate ids.txt > tweets.jsonl

API ya Twitter Masharti ya Huduma huwazuia watu kutengeza kiasi kubwa ya Twitter data ipatikane kwenye Web. Hiyo data yaeza kutumiwa kwa uchunguzi bora isi shirikiana na ulimwengu. Twitter huruhusu mafaili ya tweet identifiers kugawanywa no hiyo inaweza kuwa na manufaa. Waeza kutumia API ya Twitter ku hydrate hiyo data ama kupata kamili ya JSON. Hi ni muhimu kwa uthibitishaji ya social media research.

Watumiaji

Utumizi was users command hurudisha metadata ya majina ya skrini iliyopewa

twarc users deray,Nettaaaaaaaa > users.jsonl

Waeza pia kuipatia ids za watumiaji

twarc users 1232134,1413213 > users.jsonl

Waeza kutumia faili iliyo na ids za watumiaji kwa mfano wataka followers na friends commands

twarc users ids.txt > users.jsonl

Wafuasi

Utumizi wa followers hutegemeya follower id API ku kusanya ids za mfuasi moja kwa kila ombi. Kwa mfano:

twarc followers deray > follower_ids.txt

ita rudisha mfuasi moja kwa kila laini. Faili yako ita andikwa na wafuasi wa hivi karibuni kwanza.

Mwelekeo

Utumizi wa trends hutegemeya API ya Twitter ya mwelekeo wa hashtags. Unahitaji kuipatia Where On Earth identifier (woeid) kuiambia mwenendo unayopenda. Kwa mfano kama wataka maelekeo ya St. Louis:

twarc trends 2486982

Ukitumia woeid ya 1 itarudisha mwenendo wa dunia yote.

twarc trends 1

Ikiwa hujui nini cha kutumia ya woeid iache na utapata maeneo yote ambayo Twitter hufuata:

twarc trends

Kama una geo-location waeza kuitimia badala ya woeid

twarc trends 39.9062,-79.4679

Twitter ita tumia API ya trends/closest ili kupata woeid iliyo karibu nawe

Muda wa wakati

Utumiaji wa timeline command hutegemeya kwa API ya user timeline API kukusanya Tweets za mtumiaji alionyeshwa na screen_name:

twarc timeline deray > tweets.jsonl

Unaweza pia kuangalia juu ya watumiaji kwa kutumia id ya mtumiaji

twarc timeline 12345 > tweets.jsonl

Retweets

Unaweza kupata retweets kwa kuipeya id ya tweet hivi:

twarc retweets 824077910927691778 > retweets.jsonl

Majibu

Twitter haina API ambayo inaweza kupata majibu za tweet. twarc hujaribu kwa kutumia search API. Lakino search API haiwezi kupata majibu zaidi ya siku saba. Ikiwa unataka kupata majibu ya tweets fanya hivi:

twarc replies 824077910927691778 > replies.jsonl

Utumizi wa --recursive utapata majibu ya majibu na quotes. Hii inaweza kuchukua muda mrefu kukamilisha kama una majibu mengi kwa sababu ya kiwango cha kupunguzwa search API.

twarc replies 824077910927691778 --recursive

Orodha

Ili kupata watumiaji walio kwenye orodha unaweza kutumia URL ya orodha na command ya listmembers

twarc listmembers https://twitter.com/edsu/lists/bots

Tumia kama Maktaba

Ikiwa unataka kutumia twarc programatically kama maktaba kukusanya tweets. Kwanza utahitaji kuunda twarc instance yako. (utatumia sifa zako za Twitter), alafu utaitumia kutafuta matokeo ya utafutaji, futa matokeo au matokeo ya kufuatilia.

from twarc import Twarc

t = Twarc(consumer_key, consumer_secret, access_token, access_token_secret)
for tweet in t.search("ferguson"):
  print(tweet["text"])

Unaweza kufanya hivyo kwa mkondo wa machujio ya tweets ambazo zinafanana na kufuatilio neno muhimu:

for tweet in t.filter(track="ferguson"):
  print(tweet["text"])

au mahali

for tweet in t.filter(locations="-74,40,-73,41"):
  print(tweet["text"])

au ids za watumiaji

for tweet in t.filter(follow='12345,678910'):
  print(tweet["text"])

Vivyo hivyo unaweza ku hydrate tweet identifiers kwa kupitisha orodha ya ids au jenereta:

for tweet in t.hydrate(open('ids.txt')):
  print(tweet["text"])

Vya Kutumia

Katika saraka utils kuna commands zinazo weza kukusaidia kufanya kazi na line-oriented JSON kama kuchapisha ma tweets kwa text au html, kuchimba majina za watumiaji, URLS. If tengeneza script yako tafadhali tushirikiana na PR.

Unapopata tweets unaweza kuunda ukuta mzuri wako:

% utils/wall.py tweets.jsonl > tweets.html

Unaweza kuunda wingu ya maneno ya tweets ulizo sanya ambayo in neno nasa

% utils/wordcloud.py tweets.jsonl > wordcloud.html

Ikiwa umekusanya tweets kwa kutumia majibu unaweza kuunda taswira ya D3 na:

% utils/network.py tweets.jsonl tweets.html

Unaweza kuimarisha tweets za mtumiaji, kukuruhusu kuona akaunti kuu:

% utils/network.py --users tweets.jsonl tweets.html

Na kama unataka kutumia grafu ya mtandao katika mpango kama Gephi, unaweza kuuna faili ya GEXF na

% utils/network.py --users tweets.jsonl tweets.gexf

gender.py ni chujio kinachokuwezesha kufuta tweets kulingana na nadhani kuhusu jinsia ya mwandishi. Kwa mfano unaweza kufuta tweets zote ambazo kuangalia kama walikuwa kutoka kwa wanawake, na kuunda wingu neno na:

% utils/gender.py --gender female tweets.jsonl | utils/wordcloud.py > tweets-female.html

Unaweza kutoa GeoJSON ya tweets kama geo coordinates ziko:

% utils/geojson.py tweets.jsonl > tweets.geojson

Unaweza pia kuto GeoJSON na centriods, kubadilisha nafasi ya masanduku:

% utils/geojson.py tweets.jsonl --centroid > tweets.geojson

Na ukitoa GeoJSON na centroids, unaweza kuongeza random fuzzing:

% utils/geojson.py tweets.jsonl --centroid --fuzz 0.01 > tweets.geojson

Ili kufuta tweets kwa kuwepo au kutokuwepo kwa kuratibu za geo (au Mahali, angalia nyaraka za API):

% utils/geofilter.py tweets.jsonl --yes-coordinates > tweets-with-geocoords.jsonl
% cat tweets.jsonl | utils/geofilter.py --no-place > tweets-with-no-place.jsonl

Ili kufuta tweets na uzio wa GeoJSON (inahitaji Shapely):

% utils/geofilter.py tweets.jsonl --fence limits.geojson > fenced-tweets.jsonl
% cat tweets.jsonl | utils/geofilter.py --fence limits.geojson > fenced-tweets.jsonl

Ikiwa unadhani una duplicate kwenye tweets zako unaweza kuwapunguza:

% utils/deduplicate.py tweets.jsonl > deduped.jsonl

Unaweza kuchagua na ID, ambayo ni sawa na kutatua kwa wakati:

% utils/sort_by_id.py tweets.jsonl > sorted.jsonl

Unaweza kufuta tweets zote kabla ya tarehe fulani (kwa mfano, kama hashtag ilitumiwa kwa tukio lingine kabla ya moja unayopenda):

% utils/filter_date.py --mindate 1-may-2014 tweets.jsonl > filtered.jsonl

Unaweza kupata orodha ya HTML ya wateja kutumika:

% utils/source.py tweets.jsonl > sources.html

Ikiwa unataka kuondoa retweets:

% utils/noretweets.py tweets.jsonl > tweets_noretweets.jsonl

Au unshorten urls (requires unshrtn):

% cat tweets.jsonl | utils/unshorten.py > unshortened.jsonl

Mara baada ya kufuta URL zako unaweza kupata orodha ya vya URL inayo tweets nyingi zaidi:

% cat unshortened.jsonl | utils/urls.py | sort | uniq -c | sort -nr > urls.txt

twarc-report

Baadhi ya scripts zaidi ya huduma ili kuzalisha csv au json pato yanafaa kwa kutumia na D3.js visualizations hupatikana katika twarc-report. directed.py ilikuwa sehemu ya twarc imehama kwa twarc-report kama d3graph.py.

Kila script pia inaweza kuzalisha demo html ya taswira ya D3, kwa mfano. timelines or a directed graph of retweets.